facebookgoogle plustwitteryoutubefacebookgoogle plustwitteryoutube
Kushika Dini ni tiba ya Maradhi

Dale Carnegie

Mwandishi wa Kimarekani.

Kushika Dini ni tiba ya Maradhi

“Matabibu wa nafsi wamegundua kuwa imani madhubuti na kushikamana na dini inamtosha kushinda khofu, wasiwasi na msongo wa nafsi na kuponya maradhi haya.”

Katika wakuu wa watu (Miongoni mwa watu mashuhuri).

Michael Hart

Mwandishi wa Kimarekani.

Katika wakuu wa watu (Miongoni mwa watu mashuhuri).

“Muhammad alikuwa ni mtu wa pekee katika historia aliyefanikiwa kwa njia bora zaidi katika viwango vyote vya kidini na kidunia. Kwa hakika mkusanyiko (muunganiko) huu wa pekee ambao hauna mfano kwa ajili ya taathiri ya kidini na kidunia pamoja, linamfanya kuwa mtu mwenye haiba tukufu zaidi yenye taathira katika historia ya mwanadamu.”

Wahi Pamoja na Wasafiri

Dr.Murad Hoffman

Balozi wa Ujerumani.

Wahi Pamoja na Wasafiri

“Kuenea kwa Uislamu ni alama miongoni mwa alama zake kwenye mapito ya historia: Na hilo ni sababu hiyo ni dini ya maumbile iliyoshushwa katika moyo wa aliyechaguliwa (Mustafa).”

Dini ya watu wote.

Wagner

Mtafiti wa Kidachi (Uholanzi).

Dini ya watu wote.

“Aya mbili: “Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu….” (3:19) na “Na hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mbashiri, na mwonyaji” (34:28) zimeacha athari kubwa sana katika nafsi yangu: Kwani ndani yake kuna dalili ya ule muhuri Kilimwengu ambao Uislamu unapambauka nao mbali na zile sifa unazosifika nazo Uislamu za nidhamu na sheria nyingine na ubainifu wake kamili wa ukweli wa Nabii Issa. Je, kuna ukweli wenye nguvu zaidi kuliko mafundisho yale huru ambayo yanatuusia kuheshimu kila walichokuja nacho Mitume na manabii?! Hapana shaka yoyote kuwa dini ya Kiislamu ni dini ya haki, dini ya kweli na dini yenye hoja na dalili.”

Upekee wa Mungu mmoja (Tauhidi)

Michael Hems

Mwandishi wa Uingereza.

Upekee wa Mungu mmoja (Tauhidi)

“Hakika ya msingi katika Uislamu ni Tauhidi kuwa Allah ni mmoja na Muhammad ni Mtume wa Allah. Ama ushirikina umewekwa pembeni. Hakuna baba wala mtoto wala mpaka kati ya ambacho ni kitukufu, na ambacho ni cha dunia, au cha Mashariki na kile cha Magharibi kuna ulimwengu mmoja tu na dini moja tu.”

Haki ni Moja

-John Glenn

Mwanaanga wa kwanza wa Kimarekani

Haki ni Moja

“Kuangalia aina hii ya kiumbe wala usimuamini Mwenyezi Mungu hilo kwangu mimi ni jambo lisilowezekana ….Hili limezidisha imani yangu. Natamani pawepo na maneno yenye kuelezea tukio hili.

Miongoni mwa dalili za Utume.

Deborah Potter

Mwandishi wa Habari wa Kimarekani

Miongoni mwa dalili za Utume.

“Vipi Muhammad (mtu asiyesoma yaliyoandikwa) ambaye amekulia katika jamii ya Jaahiliya amejua miujiza ya Ulimwengu ambayo imeelezwa na Qur-aan Tukufu. Ambayo hadi hivi sasa sayansi inaendelea kuyatafiti?! Hapana shaka basi maneno haya kuwa ni maneno Mwenyezi Mungu Aliyetukuka

Falsafa na Dini.

Francis Becon

Mwanafalsafa wa Uingereza

Falsafa na Dini.

Falsafa kidogo inamsogeza mtu kwenye kumpinga Mungu. Ama kubobea katika Falsafa humrudisha mtu kwenye dini.”

Muumba wa Kila Kitu

Descartes

Mwanafalsafa wa Kifaransa

Muumba wa Kila Kitu

“Mimi nipo: Basi ni nani aliyenileta na ni aliyeniumba?, Mimi sijajiumba; hapana budi kuwepo na Muumba, na Muumba huyu hapana budi awe wajibu wa uwepo. Asiyehitaji uwepo wa mwingine aliyemleta, au mwenye kuhifadhi uwepo wake, Mungu huyu anapasa kusifika kwa sifa zote za uzuri Muumba huyu ni Allah mwanzilishi wa kila kitu.”

Tibu mwenyewe nafsi yako.

William James

Mwanazuoni wa Elimu nafsi (Saikolojia) wa Marekani.

Tibu mwenyewe nafsi yako.

“Kwa hakika tiba kubwa zaidi ya nafsi ni kumuamini Mwenyezi Mungu.”