facebookgoogle plustwitteryoutubefacebookgoogle plustwitteryoutube
Miujiza ya Ulimwengu.

Deborah Potter

Mwanahabari wa Kimarekani.

Miujiza ya Ulimwengu.

“Vipi aliweza Muhammad, mtu asiyesoma yaliyoandikwa, aliyeishi maisha zama za Ujinga aweze kujua miujiza ya Ulimwengu iliyoelezwa kwenye Qur-aan Tukufu, ambazo sayansi leo hii bado zinaendelea kushughulikia?! Bila shaka hapana budi basi maneno haya kuwa ni maneno ya Mwenyezi Mungu.”

Mungu Kumkirimu Mwanadamu

Deborah Potter

Mwanahabari wa Kimarekani

Mungu Kumkirimu Mwanadamu

Uislamu ambao ni kanuni ya Mwenyezi Mungu.Tunaona ikiwa ni wazi katika mazingira yanayotuzunguka; Kwa maamrisho pekee ya Mwenyezi Mungu, milima, bahari, sayari, nyota zinakwenda na kuongoka katika mapito yake (mzunguko wake). Vivyo hivyo kila atom katika ulimwengu huu (hata viumbe visivyokuwa hai) ila mwanadamu amevuliwa (anaondolewa) katika kanuni hii; kwani Mwenyezi Mungu amempa uhuru wa kuchagua; kwa hiyo anaweza kujisalimisha kwa amri ya Allah au akaweka kanuni zake mwenyewe na kwenda katika dini yake ambayo anairidhia, kwa masikitiko njia ya pili ina vizuizi vikubwa.”

Miongoni mwa dalili za Utume.

Deborah Potter

Mwandishi wa Habari wa Kimarekani

Miongoni mwa dalili za Utume.

“Vipi Muhammad (mtu asiyesoma yaliyoandikwa) ambaye amekulia katika jamii ya Jaahiliya amejua miujiza ya Ulimwengu ambayo imeelezwa na Qur-aan Tukufu. Ambayo hadi hivi sasa sayansi inaendelea kuyatafiti?! Hapana shaka basi maneno haya kuwa ni maneno Mwenyezi Mungu Aliyetukuka

Misingi Misafi

Deborah Potter

Mwanahabari wa Kimarekani

Misingi Misafi

“Uislamu sio dini mpya kutoka kwa Muhammad, lakini ilipoanza kusambaa ardhini baada ya kupita miaka mia sita ya kupaishwa mbinguni kwa masihi. WAHYI wa pili ulianza kushuka, ulikuwa ni ule ule unaounga dini za mbinguni na kuzirejesha kwenye asili yake safi. Mitume wote waliotumwa na Mwenyezi Mungu walikuwa Waislamu na ujumbe wao ulikuwa ni mmoja daima.”

Maneno ya Mwenyezi Mungu.

Deborah Potter

Mwandishi wa Kimarekani

Maneno ya Mwenyezi Mungu.

Nilipomaliza kusoma Qur-aan nikajawa na hisia kuwa hii ndio haki ambayo inakusanya majibu toshelevu kuhusu maumbile na mengineyo. Kadhalika hutupa matukio kwa njia ya mantiki ambayo tunaona yakigongana na vitabu vingine vya dini. Ama Qur-aan inayazungumzia kwa njia nzuri yenye kupendeza ambayo haiachi fursa ya mtu kutia shaka kuwa huu ndio ukweli, na ya kuwa maneno haya bila ya shaka ni ya Mwenyezi Mungu.