" window.dataLayer = window.dataLayer || []; function gtag(){dataLayer.push(arguments);} gtag('js', new Date()); gtag('config', 'UA-110153707-17'); " " Will Durant | 7443
facebookgoogle plustwitteryoutubefacebookgoogle plustwitteryoutube
Maadili ya Watu

Will Durant

Mwandishi wa Kimarekani.

Maadili ya Watu

“Kwa hakika Waislamu kama wanavyojulikana ni watu waliokamilika zaidi kuliko Wakristo: Walikuwa ni watu wenye kulinda ahadi zaidi, wenye kuwahurumia zaidi wanaowashinda. Na makosa machache sana waliyofanya katika historia yao kuliko unyama waliofanya Wakristo walipotawala Qudsi mwaka 1099.

Hadhi ya Mwanamke.

Will Durant

Mwandishi wa Kimarekani

Hadhi ya Mwanamke.

“Uislamu umemnyanyua mwanamke katika nchi za Kiarabu, na hivyo ukamaliza desturi ya kuua mabinti na akaweka usawa baina ya mwanaume na mwanamke katika taratibu za kisheria na uhuru wa matumizi ya mali, na akajaalia miongoni mwa haki yake ni kufanya kazi yoyote ya halali. Na kuhifadhi mali na mapato yake, kurithi na uhuru wa kutumia mali yake atakavyo, na hivyo kufuta ada waliokuwa nayo Waarabu katika zama za Ujahilia ya wanawake kurithiwa na baba zao au watoto wao kama vile zinavyorithiwa mali na mizigo, na ukafanya fungu la mirathi ya mwanamke ni nusu ya fungu la mwanaume na akakataza kuozeshwa bila ya matakwa yao.”

Dini Kwanza.

Will Durant

Mwandishi wa Kimarekani.

Dini Kwanza.

“Misingi ya tabia ya Kiislamu, sheria na serikali yao. Vyote vimesimama juu ya misingi ya dini: Uislamu ni dini nyepesi zaidi na ya wazi kuliko dini nyingine. Na msingi wake ni kushuhudia kuwa hapana Mola apasae kuaudiwa kwa haki ila Allah na Muhamad ni Mtume wa Allah.”

Nafasi ya Qur-aan na fadhila zake.

Will Durant

Mwandishi wa Kimarekani

Nafasi ya Qur-aan na fadhila zake.

“Qur-aan imebakia karne kumi na nne imehifadhiwa katika kumbukumbu ya Waislamu ikihamasisha fikra zao, kutengeneza tabia zao, na kuchochea hamasa za mamia ya milioni ya watu, Qur-aan inaweka katika nafsi za watu imani nyepesi zaidi yenye utata mchache ambao ipo mbali na vifungo vya rasimu na mafundisho ya Kikristo. Qur-aan imekuwa bora katika kunyanyua viwango vya tabia za Waislamu elimu. Na ndio iliyosimamisha ndani yao kanuni za mfumo wa kijamii na umoja wake, na kuwahimiza kufuata kanuni za afya na kufungua akili zao kutokana na dhana potofu na dhuluma na ususuavu (wa nyoyo) na kutengeneza vizuri hali za watumwa na kuingiza katika nafsi za wanyonge heshima na utukufu.”